37- Kamwingilia Mke Wake Nyuma Mchana Wa Ramadhaan - ´Allaamah Yahyaa Al-Hajuuriy

By: MirathiYaMitume

0 views

Uploaded on July 02, 2012 by MirathiYaMitume Powered by YouTube

37- Kamwingilia Mke Wake Nyuma Mchana Wa Ramadhaan - ´Allaamah Yahyaa al-Hajuuriy Swali: Mwenye kumjamii mke wake nyuma katika mchana wa Ramadhaan, je swawm yake inaharibika na inamlazimu kutoa kafara? ´Allaamah Yahyaa al-Hajuuriy: Ndio, swawm yake inaharibika bila ya khilaaf na inamlazimu kutoa kafara na huzingatiwa ni Faajir sawa ikiwa amefunga au hakufunga. Alipoulizwa Ibn ´Umar (radhiya Allaahu ´anhu) kuhusiana na kitendo hichi akasema "Ni kufuru". Mwenye kufanya hilo kwa kulihalalisha kakufuru. Na Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ "Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na MCHENI Allaah." (02:223) Kuhusiana na "Mcheni Allaah" Kataja Ibn Kathiyr (rahimahullaah) Hadiyth nyingi na Athar kuharamisha hilo na wengineo. Athar sahihi kutoka kwa Ibn ´Umar kutokana na uovu wa hili, na hapakuthibiti kauli inayoenda kinyume na hii... Amche Allaah. Lina madhara pia kama ilivyo katika "Zaad al-Ma´aad" lina madhara tendo hili chafu. Muulizaji: Vipi ikiwa atafanya lakini hahalalishi tendo hili? ´Allaamah Yayhaa al-Hajuuriy: Ni ´asi Faasiq Faajir. Wajibu kwa mke wake kutoka kwake na walii wake wamsaidie kutoka. Wakiwa na uhakika wa hilo, asiridhie yeye kwa uovu huu wala walii wake asiridhie uovu huu. Yeye kamuoza kwa Sunnah ya Allaah na Mtume wake, kamuoza kama Alivyoliruhusu Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Kasunia hilo na Kaliwekea Shari´ah kwa waja wake, na Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Manabii waliosalia walikuwa na wake na watoto. Sunnah na neema kama hii, kuikufuru ni kama mfano wa kitendo hichi. Chanzo: http://aloloom.net/show_fatawa.php?id=190
Tags:
People & Stories
Comments on 37- Kamwingilia Mke Wake Nyuma Mchana Wa Ramadhaan - ´Allaamah Yahyaa Al-Hajuuriy

RECOMMENDED CHANNELS